• TABLE OF CONTENTS
HIDE
 Front Cover
 Title Page
 Preface
 Table of Contents
 Tree growing
 The natural forests
 Questions to discuss
 Back Cover


Title: Fruits of our work
CITATION THUMBNAILS PAGE IMAGE ZOOMABLE
Full Citation
STANDARD VIEW MARC VIEW
Permanent Link: http://ufdc.ufl.edu/UF00089948/00001
 Material Information
Title: Fruits of our work women in community forestry = Matunda ya kazi yetu : wanawake na mitsitu kwa jamii, Tanzania
Alternate Title: Matunda ya kazi yetu wanawake na misitu kwa jamii, Tanzania
Physical Description: iv, 28 p. : ill., maps ; 30 cm.
Language: English
Creator: Berlekom, Maria
Food and Agriculture Organization of the United Nations
Forests, Trees and People (Program)
Donor: Marianne Schmink ( endowment )
Publisher: Food and Agriculture Organization of the United Nations,
Food and Agriculture Organization of the United Nations
Place of Publication: Nairobi
Publication Date: 1991
Copyright Date: 1991
 Subjects
Subject: Forests and forestry -- Women -- Tanzania   ( lcsh )
Women in rural development -- Tanzania   ( lcsh )
Rural development -- Women -- Tanzania   ( lcsh )
Extension -- Women -- Tanzania   ( ltcsh )
Genre: non-fiction   ( marcgt )
Spatial Coverage: Tanzania
 Notes
Statement of Responsibility: prepared by Maria Berlekom ; pictures by Charlotte Thege.
General Note: Forests, Trees and People--Cover.
General Note: English and Swahili.
 Record Information
Bibliographic ID: UF00089948
Volume ID: VID00001
Source Institution: University of Florida
Holding Location: University of Florida
Rights Management: All rights reserved by the source institution and holding location.
Resource Identifier: oclc - 27247888

Table of Contents
    Front Cover
        Front Cover 1
        Front Cover 2
    Title Page
        Page i
        Page ii
    Preface
        Page iii
    Table of Contents
        Page iv
    Tree growing
        Page 1
        Page 2
        Page 3
        Page 4
        Page 5
        Page 6
        Page 7
        Page 8
        Page 9
        Page 10
        Page 11
        Page 12
        Page 13
        Page 14
    The natural forests
        Page 15
        Page 16
        Page 17
        Page 18
        Page 19
        Page 20
        Page 21
        Page 22
        Page 23
        Page 24
        Page 25
    Questions to discuss
        Page 26
        Page 27
        Page 28
    Back Cover
        Page 29
        Page 30
Full Text
Eor~Cg51-'p1'


FRUITS
OF OUR WORK
Women in Community Forestry, Tanzania


iYIfk IIl 1 I1


1.


M~7KG6


MERGE
28


FrFRUITS


OF OUR WORK

Women in Community Forestry, Tanzania

MATUNDA


YA KAZI YETU

Wanawake na Misitu kwa Jamii, Tanzania


Prepared by:
Kimetayarishwa na:
Maria Berlekom


Pictures by:
Picha na:
Charlotte Thege
(Except number/Isipokuwa nambari:
1, 51, 90: Textslides/Picha zenye maandishi,
13, 17, 26, 36, 77, 79, 81-83: Maria Berlekom,
80, 87: Lars Johansson)


Printed by:
Kimechapishwa na:
Regal Press, Nairobi, Kenya


FOOD AND AGRICULTURE ORGANIZATION OF THE UNITED NATIONS
Nairobi, 1991All rights reserved. No part of this publication may be reproduced, stored in a retrieval
system, or transmitted in any form orby any means, electronic, mechanical, photocopying
or otherwise, without the prior permission of the copyright owner. Applications for such
permission, with a statement of the purpose and extent of the reproduction, should be
addressed to the Director, Publications Division, Food and Agriculture Organization of
the United Nations, Via delle Terme di Caracalla, 00 100 Rome, Italy.


FAO 1991


The designations employed and the presentation of material in this publication
do not imply the expression of any opinion whatsoever on the part of the
Food and Agriculture Organization of the United Nations concerning the
legal status of any country, territory, city or area or of its authorities, or
concerning the delimitation of its frontiers or boundaries.

Preface


In Tanzania, as in many other African countries, most
rural households rely heavily on trees. They use both
natural stands and planted trees for food, medicine, fuel
and building poles, and to obtain the energy and raw
materials for use in small enterprises that produce such
varied products as beer, mats and baskets.

Women are often responsible for some of the tasks which
involve use of trees. The division of household tasks
frequently assigns for example timber production to
men, leaving jobs such as fuelwood collection to women.
As a result, the interests and knowledge of women and
men differ and sometimes conflict. It is important,
therefore, to understand men's and women's roles as
they relate to forestry, and to consider the differences
when providing extension services.

This booklet and the accompanying filmstrip reveal how
extension workers in various parts of Tanzania are using
different strategies to involve men and women in forestry
activities and to insure that women benefit from extension
services to a greater extent than they have in the past. The
booklet provides the text that accompanies the slideshow
"Fruits of Our Work Women in Community Forestry,
Tanzania". Following the text, there is a section that
contains questions that can be used for discussion.

Production of the presentation was funded by the Swedish
International Development Authority and the Food and
Agriculture Organization. The work was prepared in
collaboration with the Community Forestry Section,
Ministry of Tourism, Natural Resources and
Environment, Dar es Salaam, Tanzania.


Dibaji


Nchini Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingine za
Afrika,jamii nyingi zinazoishi vijijini zinategemea sana
misitu ya asili au miti iliyopandwa, kwa kupata mazao
kama chakula, dawa, kuni na nguzo za kujengea, na pia
nishati, au mali ghafi, kwa miradi midogo midogo
iingizayo kipato, kama upikaji pombe na kutengeneza
mikeka na vikapu.

Kwa kawaida katika kila familiar kuna mgawanyo wa
uwajibikaji unaohusu matumizi ya miti. Mara nyingi
wanaume wanawajibikakwa mfano kwakazi yakutafuta
mbao, na wanawake wanawajibika kwa kazi kama
kutafuta kuni. Hii ina maana kwamba wanawake na
wanaume wanaweza kupendelea tofauti kuhusiana na
matumizi ya miti na misitu, na kwa hiyo kunaweza
kuwepo na migongano. Kwa hiyo ni muhimu sana
kuelewa majukumu ya wanawake na wanaume
yanayohusu miti na misitu, na kuyaangalia haya katika
kazi zote za uenezi misitu kwa jamii.

Kijitabu hiki kinaonyesha ni jinsi gani wafanyakazi wa
uenezi katika sehemu mbalimbali za Tanzania
wanavyotumia mikakati mbalimbali ya kuwashirikisha
wanawake na wanaume katika shughuli za misitu, na
jinsi gani wanawasaidia wanawake kunufaika zaidi na
kazi za uenezi misitu. Kijitabu kinatoa maneno ya
wazungumzaji wa Sinema ya Picha "Matunda ya Kazi
Yetu Wanawake na Misitu kwa Jamii, Tanzania".
Mwisho wa kijitabu kuna sehemu ya maswali kwa ajili
ya majadiliano.

Sinema ya Picha ilihisaniwa na Shirika la Sweden la
Maendeleo ya Kimataifa (SIDA) pamoja na Shirika la
Kilimo na Chakula Duniani (FAO), na kimetayarishwa
kwa ushirikiano pamoja na Kitengo cha Misitu kwa
Jamii, Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Utalii,
Maliasili na Mazingira, Dar es Salaam, Tanzania.AFRICA


TANZANIA


*Areas visited
Sehemu zilizotembelewa


CONTENTS


Preface
Maps
Contents

Speaker's Notes to the Slideshow:
Part I: Tree Growing
- Introduction
- Mgeta: Where men plant a lot of trees
- Dodoma: Where some women may not
plant trees
- Arusha: Where wife and husband
cooperate

Part II: The Natural Forests
- Morogoro: Where villages make
woodland management plans
- Morogoro: Where women benefit
from charcoal saving stoves
- Babati: Where women protect their
sacred forests
- Final words

Questions to discuss
YALIYOMO

Dibaji
Ramani
Yaliyomo

Maneno ya Wazungumzaji:
Sehemu ya Kwanza: Uoteshaji Miti
- Utangulizi
- Mgeta: Wanaume wanapanda miti mingi
- Dodoma: Wanawake wanapata
shida kupanda miti
- Arusha: Mke na mume wanashirikiana


Page
iii
iv
iv


Ukurasa
iii
iv
iv1
1
4

8
12


Sehemu ya Pili: Matumizi Bora ya Misitu ya Asili
- Morogoro: Vijiji vinapanga matumizi
bora ya misitu yao
- Morogoro: Wanawake wananufaika
kutokana na majiko sanifu
- Babati: Wanawake wanalinda
misitu yao ya kimila
- Maneno ya mwisho

Maswali ya kujadiliFirst Part: Tree Growing


Sehemu ya Kwanza: Uoteshaji Miti


Introduction
Utangulizi


1. Matunda ya Kazi Yetu Wanawake na Misitu kwa
Jamii, Tanzania.
1. Uoteshaji miti.


2. Damarifrom Arusha: "This orange tree I planted
some years ago. I have planted fruit trees in our home
garden on and off since I married and moved here."

2. Damari kutokaArusha: "Mchungwa huu nilipanda
miaka mitano iliyopita. Nimepanda miti ya matunda
karibu na nyumbani mara kwa mara tangu nimeolewa na
kuhamia hapa."


3. "The local forester has been very helpful and has
advised both me and my husband on how to grow and
take care of trees."

3. "Na Bwana Miti wetu ametushauri mimi na mume
wangu jinsi ya kuotesha miti na kuitunza."


4. Speaker: "Tanzania is a country, rich in forests and
woodlands..."

4. Mzungumzaji: "Tanzania ni nchi yenye misitu
mingi kama vile miombo, nyika, vichaka na kadhalika..."


Introduction
Utangulizi


5. "...but in many places these have disappeared, and
tree products are hard to find. This affects both men and
women..."

5. "...lakini sehemu nyingi sasa misitu hii imepotea na
imekuwa vigumu kupata mazao ya misitu. Hii inaleta
matatizo kwa wananchi wote, wanaume na wanawake."


6. "...and calls for action."


6. "Kwahiyohatuayakurekebisha halihiiinahitajika."


7. "But sometimes women find it difficult to participate,
or might not benefit from their own efforts."

7. "Lakini wakati mwengine wanawake wanaona
vigumu kushiriki, kwa vile hawana uhakika wa kufaidika
kutokana na jitihada zao."


8. "I am Hadija Ramadhani, and I am working at the
Forest and Beekeeping Division in Dar es Salaam. My
work is to ensure that women will benefit from forestry
extension activities."

8. "Mimi, naitwa Hadija Ramadhani, na nafanya kazi
katika Idara ya Misitu na Nyuki, Dar es Salaam. Kazi
yangu ni kusaidia wanawake kufaidika kutokana na
shughuli za kimisitu."


Introduction
Utangulizi


9. "In this slideshow, we want to show a few examples
from different parts of Tanzania on how women with
help from extension workers, either alone..."

9. "Katika sinema hii tunataka kuonyesha mifano
kutoka sehemu mbalimbali Tanzania. Tutaona jinsi
Maafisa Misitu wanavyoweza kusaidia wanawake
binafsi..."


10. "...or together with husbands, other women and
village communities have been able to increase women's
access to tree and forestry products."

10. "...au kusaidia wanawake pamoja na wanaume wao,
wanawake engine, au Serikali za vijiji, kuongeza
upatikanaji wa mazao yatokanayo na miti na misitu."


11. "This first part is about tree growing. We will see
some different ways of helping women and the whole
family to benefit from growing trees."

11. "Katika sehemu hii ya kwanza tutaona mbinu tofauti
zinazotumika katika kuhusisha wanawake pamoja na
jamii nzima katika swala zima la uoteshaji miti."

The Forester's Story
Hadithi ya Bwana Miti


Mgeta: Where Men Plant a
Lot of Trees

Mgeta: Wanaume Wanapanda

Miti Mingi


12. Speaker: "Our first example is from Mgeta Division
high up in Uluguru Mountains, where traditionally mainly
men plant trees."

12. Mzungumzaji: "Mfano wetu wa kwanza ni kutoka
Tarafa ya Mgeta iliyopo katika Milima ya Uluguru,
ambapo wanaume ndiyo wanaopanda miti mingi."


13. The forester: "I am Alfred Ng'atigwa. I was born in
Mgeta Division, and I'm Divisional Forester here."

13. Bwana Miti: "Mimi ninaitwa Alfred Ng'atigwa.
Nimezaliwa Tarafa ya Mgeta, Kata ya Kikeo. Mimi ni
Bwana Miti wa Tarafa hapa Mgeta."


14. "In Mgeta Division there are no unprotected natural
forests to use, so many people have planted their own
trees in their own fields."

14. "Hapa Tarafani Mgeta hakuna msitu wa asili ambao
unaweza ukamwezesha mwananchi ye yote akaenda
msituni akaokota kuni. Kwa hiyo kila mtu anajipandia
miti mwenyewe katika shamba lake..."


- MMgeta


15. "And both tree planting and felling is usually done by
men. This way they provide the household with all tree
products needed, including firewood. This is the tradition
of old."

15. "...na anakwenda kukata miti ya kwake, na hasa
akinababa upandaji miti kazi yao, na ukataji miti. Hii
mila na desturi tangu zamani."


16. "I don't think it is very necessary to stress a lot that
women should plant trees also as plenty of trees are
planted anyway by men."

16. "Kwahiyo akinababa wanapanda miti sanakutokana
na matumizi mbalimbali, kama vile kupata kuni kwa
matumizi ya nyumbani na kupata majengo na mbao."


17. "Instead I mainly advise women to start farm tree
nurseries. Then their husbands can plant trees, or the
women can sell the tree seedlings to other men, and get
some money."

17. "Kwa hiyo kwa upande wa akinamama zaidi
tunawashauri kuanzisha vitalu vya miti, kwa sababu ni
kazi inayofaa kuifanya nyumbani bila kupoteza muda
mwingi na kwenda mbali. Wanastawisha vitalu, na miti
ikiwa tayari wanauza kwa akinababa."


The Old Man's Story
Hadithi ya Mzee Alexi


18. The old man: "I am Alex Mkamwa. I live in Langali
village here in Mgeta. I am a farmer."

18. Mzee Alexi: "Mimi Alexi Mkamwa. Mimi niko
katika kijiji cha Langali hapa Mgeta. Shughuli zangu
k.,lima."Mgeta


pE. ':


19. "I started to plant trees here 1943, following the
examples of my older relatives. Now in total I have one
acre."

19. "Nina ekari moja ya miti. Nimeanza kupanda miti
hapa 1943."

20. "I took wild-
lings growing on
land belonging to
my clan. Last
time I planted
was last year.
These are the
trees"

20. "Nilipata
kwa wazee ka-
tika mashamba
ya ukoo wetu,
ndiko nili-
kokwenda ku-
ng'oa, ndiyo
napandikiza sha-
mba hili. Mwisho
wa kupanda
mwaka jana."


21. "What made me start was our need. My wife needed
firewood for cooking. I wanted building poles to build
houses for the family. Also I wanted to sell timber."

21. "Kilichonifanya, maisha yangu, mambo ya kuni,
nisipate taabu. Kuni, pamoja na kuuza boriti, pamoja na
kupasua mbao."
Amanda's Story
Hadithi ya Amanda


22. Amanda: "My name is Amanda Bethy. I live with
my husband and six children in Langali village, in Mgeta
Division. I am a farmer."

22. Amanda: "Jina langu Amanda Bethy. Ninaishikatika
kijiji cha Langali, Mgeta. Nina mume na watoto sita na
pia ni mkulima."


IMgeta


23. "I started
my tree nursery
two years ago.
The work in the
nursery is done by
me, with help of
my children. My
husband will plant
the trees once it
starts to rain."

23. "Nilianza
shughuli za
ukuzaji miche
miaka miwili
iliyopita. Kazi ya
bustani naifanya
mimi pamoja na
watotowangu. Na
mume wangu ndiyo ni yule atakayepanda miti hii mvua
itakapoanza kunyesha."


24. "The trees he doesn't plant, I sell to my neighbours
for 15 shillings, and I have seen that mainly men come
to buy."

24. "Miche mingine inayobaki nauza kwa majirani kwa
Shs 15/- kila mche, na nimeona wanaonunua wengi ni
wanaume."


25. "This year I raise 200 seedlings. People like to buy
fruit trees like guava, passion fruit and papaya. They also
like trees for timber and building poles, like Grevillea
and Eucalyptus."

25. "Mwakahuu nimekuza miche 200. Watu wanapenda
kununua miche ya matunda kama vile mipera, mipapai
na mipassion. Pia wanapenda miti ya mbao na majengo
kama vile Grevillea na Mikaratusi."


26. "The local forester helps anyone who wants to start
a tree nursery with advice, and sometimes also with
seeds and polythene tubes."

26. "Bwana Miti wetu anasaidia kila mmoja anayetaka
kuanzisha bustani ya miti kwa kutoa ushauri. Vilevile
mara kwa mara anatusaidia na viriba na mbegu."


Mgeta


27. "I think
AS"that this kind of
Tt work is very
suitable for
A !women. I don't
have to go away
and leave the
children, it is not
heavy. Also it is
good because I
get some
S.u money."

27. "Nafikiri
kaziyaainahiini
nzuri kwa
akinamama, kwa
vile siendi mbali
na nyumbani na kuacha watoto, na sio ngumu. Vilevile
ni nzuri kwa sababu napata fedha."


Dodoma:


Where Some
Women May Not
Plant Trees


Dodoma: Wanawake
Wanapata Shida
Kupanda Miti


_ Nt-.,ip as-"o;:s .*--ssss^"""' ^^^"
28. Speaker: "In the semi-arid Dodoma area some
women find it hard to plant trees."

28. Mzungumzaji: "Mfano wetu wa pili unatoka
Dodoma ambao ni mkoa nyanda kame. Hapa baadhi ya
wanawake wanaona ni shida kupanda miti."


Dodoma


The Community Development Worker's Story
Hadithi ya Bibi Maendeleo


>.~,vJ .'
Vt~


29. The Community Development Worker: "My name
is Monica Mhavile. I am a Community Development
Officer assigned to DOVAP, or the Dodoma Village
Afforestation Project. We work in villages in Dodoma
urban District."

29. BibiMaendeleo: "Jina langu ni Monica Mhavile. Ni
Afisa Maendeleo ya Jamii, nafanya kazi DOVAP, au
Mradi wa Upandaji Miti Dodoma. Tunafanya kazi katika
vijiji vya Wilaya ya Dodoma mjini."


30. "In the beginning we made no efforts to reach
women, and often our fieldworkers forgot to speak to
women when they visited peoples homes."

30. "Tulivyoanza mradi huu hatukuweka mkazojinsi ya
kuwafikia akinamama, na mara nyingi Mabwana na
Mabibi Miti wetu vijijini walisahau akinamama wakati
walipotembelea watu majumbani kwao."


31. "Therefore we decided to let the fieldworkers do a
small survey, and interview women: both to make them
see women, and to get to know more about women's
problems and needs."

31. "Kwa hiyo tuliamua wafanye utafiti kidogo wa
kuhoji akinamama, ili wawakumbuke akinamama zaidi,
na pia kuweza kujua matatizo na mahitaji yao."


32. "This way we learnt that some women are not
allowed by their husbands to plant trees. And a woman
who plants, risks seeing her husband taking all benefits
for himself."

32. "Kwa njia hii tuliweza kujifunza kwamba kuna
baadhi ya wanawake hawaruhusiwi na waume wao
kupanda miti. Na hata mwanamke akipanda miti
anayefaidi matunda ni mume wake peke yake."Dodoma


Hadithi ya Jemima
Jemima's Story


33. "Then we decided to have local meetings for women,
and encourage them to start tree growing groups."

33. "Kwa hiyo tuliamua kufanya mikutano kwa
akinamama peke yao, na kuwashauri kuanza kuotesha
miti kwa vikundi."


34. "We also try to raise awareness among men about
importance of tree planting for the benefits of the whole
household, like nutritional values of fruits for children."

34. "Vile vile tunajaribu kuhamasisha wanaume kuhusu
umuhimu wakuoteshamiti kwa manufaa yajamii nzima,
kama vile kupata lishe bora ya matunda kwa watoto."


35. Jemima: "Jemima Enock is my name. I am a farmer
here in Ntyuka, Dodoma. I have four children. For many
women in Ntyuka it is a big problem to plant trees,
because our husbands decide over us."

35. Jemima: "Jina langu ni Jemima Enock. Ni mkulima
hapa Ntyuka, Dodoma, na nina watoto wanne. Kwa
wanawake wengi hapa Ntyuka ni tatizo kubwa kupanda
miti, kwa sababu wanaume wetu wanauamuzijuu yetu."


36. "If I plant fruit trees my husband can take the fruits
and sell them. Then the children won't get the fruits..."

36. "Kama tukipanda miti ya matunda wanaume wetu
watachukua matunda na kwenda kuuza. Halafu watoto
watakosa matunda..."


. IDodoma


37. "...and I will probably not see the money. And some
other women are not even allowed to plant trees at
home."

37. "...na hata pesa hataleta nyumbani. Na akinamama
engine hawaruhusiwi kupanda miti nyumbani kwao."


I -K-


Maps.~
ON


38. "To help us the local forester called a meeting and
advised us to start a women's tree growing group. We
have already three acres which we were given from the
Village Government, and on these we have planted fruit
trees."

38. "Kwa hiyo Afisa Msitu wetu alitushauri kuanzisha
kikundi cha akinamama cha kuotesha miti. Tayari
tunazo eka tatu, ambazo tulipata kutoka Serikali ya kijiji,
na tumeshapanda miti yamatundakwakutumiamapingili
na miche."


39. "Now we water our trees every day, and each group
member has to take her turn with the watering."

39. "Na sasa tunamwagilia miti hii maji kila siku, na kila
mwanakikundi lazima aje na kufanya kwa zamu yake."


40. "Our forester also helps us to convince our husbands
to grow and plant trees at home."

40. "Pia yule Afisa Msitu anajaribu kuhamasisha
wanaume wetu kutusaidia kuotesha miti nyumbani."
The Forester's Story
Hadithi ya Bwana Miti


Arusha: Where Wife and
Husband Cooperate

Arusha: Mke na Mume
Wanashirikiana


41. Speaker:
"In the Arusha-
area people have
for many years
been inter-
planting many
different trees
with other crops,
in a local agro-
forestry system.
Land is scarce
and plots are
small so the
diversity helps to
increase prod-
uction from the
plots."


41. Mzungumzaji: "Katika sehemu zajuu za Wilaya ya
Arumeru kwa miaka mingi watu wamekuwa
wakichanganya mazao ya chakula na miti, ili wapate
mazao mengi tofauti na kupata mavuno makubwa kutoka
sehemu moja."


42. The forester: "My name is Fadhili Sechonge and I
am working in Muklat Division in Arumeru District. I
think it is important to talk with both women and men, as
the household is a unit where husband and wife have
different roles, but still usually cooperate."

42. Bwana Miti: "Jina langu ni Fadhili Sechonge,
nafanya kazi katika Tarafa ya Muklat, Wilaya ya
Arumeru. Katika kazi yangu lazima kuongea na
wanawake na wanaume pamoja, kwa vile kawaida wana
wajibu tofauti katika jamii lakini hata hivyo bado
wanashirikiana."


43. "I have seen that often women are particularly
interested in planting fruittrees in the home gardens near
the houses, both to get fruits to sell and to get nutritious
food for children."

43. "Nimeona kwamba akinamama mara nyingi
wanapenda hasa kupanda miti ya matunda karibu ya
nyumba zao, ili waweze kuuzapamoja na kupata chakula
bora kwa watoto wao."


Arusha


44. "But men, like this young man, prefer to plant trees
for building poles and timber."

44. "Na wanaume, kama huyu kijana, kawaida
wanapenda zaidi kupanda miti kwa ajili ya majengo
pamoja na kupata mbao."


Damari's and Nestor's Story
Hadithi ya Damari na Nestor


45. Damari: "I am Damari Ole, I live in Oldonyowass
village, Arusha, with my husband and our four children."

Nestor: "My name is Nestor Ole. I am a farmer."

45. Damari: "NaitwaDamari Ole. Naishihapakijijicha
Oldonyowassi pamoja na mume wangu na watoto wetu
wanne."

Nestor: "Jina langu ni Nestor Ole, na ni mkulima."


46. Damari:
"This avocado
tree Iplanted five
years ago. I have
planted fruit trees
in our home
garden on and off
since I married
and moved here."

46. Damari:
"Mti huu
nilipanda miaka
mitano iliyopita.
Nimepanda miti
ya matunda
karibu na
nyumba yangu


tangu nimeolewa na kuhamia hapa."


47. Nestor: "The timber I will sell when the trees are
mature, so we will get a good piece of money. We prune
the trees yearly and so get a lot of firewood."

47. Nestor: "Mbao nitakazouza wakati miti
itakapokomaatutapatakipato kizuri sana. Tunapunguzia
miti hii matawi kila mwaka kwa hiyo tunapata kuni
nyingi sana."
48. Damari: "My husband planted Leucaena as fodder
for our three cows. This makes it easier for me in my
work to collect fodder."

48. Damari: "Mume wangu amepanda Lusina kwa ajili
ya chakula cha ng'ombe wetu. Hii hunirahisishia kazi ya
kutafuta majani ya ng'ombe mbali."


benki ambayo huongezeka ili sisi
tutatumia tukipata matatizo."


49. Nestor:"I
have planted the
trees also to have
as insurance for
the future. The
trees are like a
bank account
growing, that we
and our children
will use if we get
trouble."

49. Nestor:
"Nimepandamiti
pia kwa ajili ya
akiba yetu ya
baadaye. Miti ni
kama akaunti ya
na watoto wetu


50. Damari: "I like our forester because he cooperates
with both me and my husband. After all, women and men
are all Gods people, and in the household we have to
work side by side."

50. Damari:"Bwana Miti wetu ni mtu mzuri kwa sababu
anashirikiana na mimi na mume wangu kwa pamoja. Na
kweli wanawake na wanaume sisi wote ni watu wa
Mungu, na katika nyumba lazima tufanye kazi pamoja
au bega kwa bega."


Arusha


Second Part: The Natural Forests


Sehemu ya Pili: Matumizi Bora ya

Misitu ya Asili


51. Speaker: "The second part of this slideshow shows
how women can contribute to protection and sustainable
utilization of natural forests."
51. Mzungumzaji: "Katika sehemu hii ya pili tutaona
akinamama wanavyoweza kupunguza upotevu wa misitu
ya asili, na vilevile kufaidika kutokana na matumizi bora
ya misitu."


Morogoro:Morogoro:


Where the Villages
Make Woodland
Management Plans

Vijiji Vinapanga
Matumizi Bora ya
Misitu Yao


52. Speaker: "In this example from Morogoro we will
see how women can benefit from an appropriate use of
woodland areas."
52. Mzungumzaji: "Hapa Morogoro baadhi ya vijiji
vimeshaanza kupanga matumizi bora ya misitu ya asili,
ambayo inasaidia sana akinamama."


Morogoro


The Forester's Story
Hadithi ya Bibi Miti


53. The forester: "Neema Dugilo is my name, and I am
a forestry extension worker, working in Morogoro
District."

53. Bibi Mit: "Jina langu ni Neema Dugilo. Mimi ni
Bibi Miti, na nafanya kazi na Wilaya ya Morogoro."


54. "In areas where natural forests are still quite plenty
we help villages to plan a proper use of these, before the
forests have been cut down. This is much cheaper and
easier than having to reafforest later."

54. "Katika sehemu ambazo bado zina misitu mingi ya
asili tunasaidia wanavijiji kupanga matumizi bora ya
misitu hio, kabla ya misitu hii kutoweka. Njia hii ina
gharama kidogo nakazi kidogo kuliko kujakupanda miti
tena baadaye."


55. "It also
ensures women
access to all
products they
collect from
woodland areas.
Thus women's
workload will not
increase, neither
through in-
creased distances
'- to firewood
o sources, nor
S throughhavingto
plant trees."

S55. "Vilevile
inahakikisha
upatikanaji wa mazao ya misitu yanayotumiwa na
akinamama. Kwa hiyo kazi za akinamama
hazitaongezeka, kwa sababu hawatalazimika kuokota
kuni mbali, wala kulazimika kupanda miti."


56. "Uses that do not destroy the forests can be allowed
- such as gathering of fibres for making baskets, firewood
collection for household use and beer brewing, and
collection of nuts, leaves, grasses, and medicines."

56. "Matumizi ambayo hayaharibu misitu yanaweza
kuruhusiwa, kama vile kukusanya ukindu, matunda pori,
madawa, kukata majani, na uokotaji wa kuni kwa
matumizi ya nyumbani na upikaji wa pombe."


Morogoro


Christophina's Story
Hadithi ya Christophina


57. "Whereas uncontrolled grazing, clearing of land,
charcoal burning, and commercial tree felling deplete
the woodlands, and therefore need to be restricted."

57. "Matumizi engine yanamaliza misitu ya asili, na
yanahitaji kuzuiliwa, kama vile uchungaji holela, upanuzi
wa mashamba, uchomaji mkaa na ukataji miti kwa ajili
ya biashara."


58. "In two villages, Melela and Kiroka we arranged
seminars for village leaders, and discussed the issue.
This resultated eventually in both villages adopting their
own village bylaws."

58. "Katika vijiji vya Melela na Kiroka tuliendesha
semina kwa viongozi wa vijiji na kuongelea swala hili.
Matokeoyake yabaadaye, nikwambakilakijijikilitunga
sheria ndogo ndogo kuhusu matumizi bora ya misitu ya
asili kijijini."


59. Christophina: "Me, I'm Christophina Edward
Kibindu. I'm a farmer in Kiroka village, and I live in my
father's house with my children."

59. Christophina: "Mimi ni Christophina Edward
Kibindu. Ni mkulima katika kijiji cha Kiroka, na naishi
katika nyumba ya baba yangu pamojana watoto wangu."


60. "We women get many things from the natural forests;
we collect firewood for cooking and for beer-brewing,
and we gather edible plants, leaves and fruits."

60. "Sisi akinamama tunapata vitu vingi kutoka misitu
ya asili, kama vile kuni kwa ajili ya kupika na kutengeneza
pombe, na ukindu kwa kutengenza mikeka na vikapu."


I


Morogoro


61. "There used to be plenty of forests close to the
village, but now we have to walk up the hill. Still,
firewood we find in plenty, even if some forests disappear
every year."

61. "Zamani kulikuwa na misitu mingi karibu na kijiji,
lakini sasa tunapandisha mlimani. Hata hivyo, kuni bado
nyingi, ingawa misitu inapungua kila mwaka."


62. "But it's not we women who destroy the forests,
because we prefer to collect dry and fallen branches, or
to cut small branches, but not to fell whole trees. To
secure our firewood sources the Kiroka Village
Government therefore adopted a village by-law:"

62. "Lakini sio sisi akinamama tunaoharibu misitu, kwa
sababu sisi tunapendeleakukusanya matawi yaliyokauka
na kuanguka, au kukata matawi madogo tu, lakini sio
kuangusha miti mikubwa. Ili kutusaidia kabla ya misitu
hii ya asili kutoweka Serikali ya kijiji ya Kiroka
ilitengeneza sheria ndogo ndogo..."


63. "In each sub-village at least five acres of woodlands
are set aside. In these areas all uses that destroy the forest
are forbidden, such as clearing new land for cultivation."

63. "...kwamba katika kila kitongoji zitengwe sio chini
ya eka tano ya misitu ya asili. Katika maeneo haya
matumizi yanayoharibu misitu yanazuiliwa, kama vile
ufyekaji kwa ajili ya kilimo."


64. "But we women are allowed to continue collecting
the products we always have gathered: herbs, fibres,
leaves, wild fruits, edible plants and firewood."

64. "Lakini sisi akinamama tunaruhusiwa kuendelea
kupata mazao ya misitu kama vile madawa, mboga
mboga za jadi, majani, kuni, ukindu, matunda n.k."65. "The village adopted this by-law after many meetings,
where both men and women could say what they thought
about the problem of our disappearing forests."

65. "Kijiji kilitunga sheria hizi ndogo ndogo baada ya
mikutano mingi, ambapo wote wanaume na wanawake
waliweza kutoa maoni yao kuhusu swala hili."


66. "And two women are members of the village forestry
committee. This committee supervises management of
the 40 acres of woodlands that are protected by the by-
law."

66. "Na akinamama wawili walichaguliwa kuwa
wajumbe wa kamati ya misitu ya kijiji. Kamati hii
inaangalia utunzaji wa zile eka 40 zinazolindwa na
sheria zetu ndogo ndogo."


Morogoro: Where Women
Benefit from
Charcoal Saving
Stoves


Morogoro:


Wanawake
Wananufaika


Kutokana na
Majiko Sanifu


67. Speaker: "Charcoal burning is one of the things that
can destroy the forest. This example, which is also from
Morogoro..."

67. Mzungumzaji: "Uchomaji mkaa bila mipango ni
mojawapo wa matumizi yanayoharibu misitu. Mfano
huu unaotoka Morogoro..."Morogoro


68. "...shows how both village and townliving womencan
help to reduce charcoal consumption and at the same
time benefit from either production or utilization of
charcoal saving stoves."

68. "...unaonyesha wazi kwamba akinamama kweli
wanaweza kupunguza matumizi ya mkaa, na vilevile
kufaidikawenyewe kutokana nakutengenezanakutumia
majiko sanifu ya mkaa."


The Stove Extensionist's Story
Hadithi ya Mama Majiko


69. The Stove Extensionist: "I am called Rehema
Kizulege, and my work in the Morogoro Fuelwood
Stove Project is to dissiminate fuelwood saving stoves..."

69. Mama Majiko: "Mimi naitwa Rehema Kizulege.
Kazi yangu katika Mradi wa Majiko wa Morogoro ni
kufundisha akinamama kuhusu utumiaji wa majiko
sanifu..."


70. "...and to teach village women about producing
stoves in small income generating projects."

70. "...pamoja na jinsi ya kutengeneza majiko haya ya
mkaa ya kuuza."


71. "We teach two types of stoves: A fixed mudstove for
firewood, called the Kilakaka stove..."

71. "Tunafundisha aina mbili za majiko. Jiko la matope
la kutumia kuni, linaloitwa jiko la Kilakala..."


I


Morogoro


72. "...and a portable stove for charcoal, called the
Morogoro stove. The charcoal stove is most popular,
both among producers and users."

72. "...na jiko la Morogoro la mkaa, ambalo ni rahisi
kubeba. Jiko hili la mkaa hupendwa zaidi na wote,
watengenezaji pamoja na watumiaji."
Hadija's Story
Hadithi ya Hadija


73. Hadija:"I am Hadija Omari. I live here in Morogoro
town with my husband and five children."

73. Hadija: "Mimi ni Hadija Omar. Naishi Morogoro
mjini pamoja na mume wangu na watoto wetu watano."


9'
--i


~^


74. "Previously I used an ordinary charcoal stove together
with a kerosene stove. They really consumed much
charcoal and kerosene every month, so a lot of money
was spent."

74. "Zamani nilikuwa natumia jiko la kawaida la mkaa
pamoja na jiko la Mchina. Majiko haya yalitumia mkaa
na mafuta mengi kila mwezi, kwa hiyo fedha zilipungua
haraka."


75. "Some years
ago I saw my
neighbours using
this Morogoro
charcoal stove,
and they told me
that it is very
good; it cooks
fast, and uses
very little
charcoal. So I
decided to buy
one."


S.75. "Miaka ya
nyuma kidogo
niliona jirani
zangu wakitumia jiko la Morogoro, na waliniambia ni
jiko zuri: chakula kinaiva haraka, na kutumia mkaa
kidogo tu. Basi nikaamua kununua moja."


__


Morogoro


76. "I went to the market and bought it for 250 shillings,
which was cheaper than the ordinary charcoal stove."

76. "Nilikwenda sokoni na kununua kwa shilingi 250,
ambayo ilikuwa bei nafuu kuliko lile jiko la mkaa la
kawaida."


77. "I like the stove very much. Every month it uses
much less charcoal, so I remain with more money for
buying food, clothes and raise the children well."

77. "Napendajiko hili sana. Kila mwezi linatumia mkaa
kidogo. Kwa hiyo nabaki na pesa zaidi kwa kununua
chakula na nguo, pamoja na kulea watoto vizuri."


Babati: Where Women Protect
their Sacred Forests


Babati: Wanawake Wanalinda
Misitu yao ya Kimila


78. Speaker: "In Rirodavillage, Babati, the local forester
has realized the importance of respecting old beliefs and
traditions concerning trees and forests."

78. Mzungumzaji: "Katika kijiji cha Riroda, Babati,
Bwana Miti ameelewa umuhimu wa kuheshimu mila na
desturi za zamani kuhusu miti na misitu."


J- -i.

ri4Ki-


Babati


The Forester's Story
Hadithi ya Bwana Miti


79. The forester: "I am Laurence Mkanwa, forester in
Riroda and Duru Wards. There are three types of protected
forests in Riroda: Government Forest Reserves,
traditional forests of men and also women's sacred
forests."

79. Bwana Miti: "Mimi naitwa Laurence Mkanwa, ni
Bwana Miti wa Kata Riroda na Duru. Ulinzi wa misitu
ya asili umegawanyika katika sehemu tatu kubwa.
Kwanza kabisa kuna misitu ya Serikali ambayo ni ya
Halmashauri."


80. "There are ten sacred forests of men in Riroda, each
being about one and a half acre big."

80. "Halafu misitu ya akinababa wa kabila Wagorowa,
ambayo inaitwa ghai-manda. Halafu kuna misitu ya
akinamama, ambayo inaitwa ghai-dessu. Upande wa
akinababa wana misitu karibu kumi katika eneo la
Riroda, na kila msitu unakadiriwa kuwa kama eka moja
na nusu."


81. "Traditional forests of women are smaller about
a quarter of an acre and in total there are three."

81. "Na ya akinamama ni kama robo moja eka, na misitu
yao iko mitatu katika eneo hili la Riroda."


82. "The tra-
ditional forest
reserves are abig
help in my work
to protect the
environment.
People respect
them, and
anybody who
does anything to
destroy a sacred
forest is punished
and fined by the
S group who is in
i charge of that
particular
forest."

82. "Misitu hii ya kimila inanisaidia sana katika ya
kuhifadhi mazingira. Maana yake, inaheshemiwa kwa
sababu wenyewe huwa wanafanya shughuli zao, na mtu
hawezi kuharibu msitu huu."


Babati


The Old Woman's Story
Hadithi ya Bibi Martha


83. The old woman: "My name is Martha, Martha
Ghera. I am a farmer here in Riroda and I have many
children and grandchildren."

83. BibiMartha: "Mimi ninaitwa Martha, Martha Ghera,
na shughuli yangu hapo Riroda ni kulima. Nina watoto
na wajukuu wengi sana."


84. "This forest is called ghai-dessu, or the forest of
young women. The laws of the forest say: no trees are to
be cut, no wood to be collected and no man ever to
come here."

84. "Msitu huu unaitwa ghai-dessu. Kwa kiswahili ni
msitu wa wasichana. Sheria ya msitu huu ni kwamba:
isikatwe miti yo yote na isiingie kijana wo wote wa
kiume hapa."


85. "Anybody who breaks the law has to pay a bull, a bull
to be slaughtered for us women."

85. "Faini yake tunamtoza dume, dume la ng'ombe,
mpaka lichinjwe kwa akinamama."


86. "Those who guard the forest are the young women,
they are the ones who do ceremonies here. This started
long time ago, when our ancestors were young."

86. "Wanaotunza msitu huu zaidi ni wasichana, ndiyo ni
wasichana na wanawake wanaoshughulikia hapa. Hii
ilianza muda mrefu. Sisi tulikuta waliotutangulia, mpaka
sasa bado inaendelea."
Final Words
Maneno ya Mwisho


87. "Our forester is a good man, because he respects our
old traditions and listens to our own leaders, and for
example often takes advise from our local healer,
Quashan. Therefore we villagers listen to him and agree
when he talks about why also Government Forest
Reserves should be respected."

87. "Yule Bwana Miti wa hapa tunampenda. Mara kwa
mara anakwenda na kupata mashauri kutoka mganga
wetu, mzee Quashan. Kwa hiyo anatusikiliza na
kuheshimu mila zetu. Kwa hiyo sisi wanakijiji
tunamsikiliza vizuri na kumuelewa anapozungumzia
umuhimu wa kuhifadhai misitu ya Serikali vilevile."


88. Speaker: "We have now seen that there are many
ways of involving women in forestry activities. What is
best in each area will of course depend on local conditions,
and what both women and men say they need and like to
do."

88. Mzungumzaji: "Tumekwishaonakwambakunanjia
nyingi tofauti za kusaidia akinamama wafaidike kutokana
na shughuli za kimisitu. Katika kila sehemu ni muhimu
kutegemea na hali halisi ya pale mahali. Kwa hiyo kitu
cha awali ni kukaa na kuongea na wote, wanaume na
wanawake."


89. Woman from Dodoma: "What I like best with the
forestry officers coming here is that they listen to both
women and men, and that way try to find solutions to our
forestry problems that are accepted by everybody."

89. Mwanamke kutoka Dodoma: "Ninachompenda
Bwana Miti wetu ni kwamba akija anaongea na sisi
wote, akinamama na akinababa. Kwa njia hii anajaribu
kutatua matatizo ya kukosa mazao, yanayotokana na
miti na misitu, kwa njia zinazopendwa na watu wote."
Questions to Discuss


The following questions are intended as a help to those
who are using the slideshow as a teaching and training
material. They are most suitable for discussions in small
groups, during for example seminars and courses for
extension workers.PART I: TREE GROWING

1. Discuss and analyze the three cases presented (Mgeta,
Dodoma and Arusha):

a) What tree and forestry products are lacking and seem
to be needed in each area?

b) What are the traditions concerning tree growing and
tree planting 1) of men 2) of women in each area?

c) What species (or kind of trees) do farmers (men and
women respectively) generally seem to prefer?

d) Do women have access to all tree products they need
and are supposed to provide for the household?

e) Is there a need for women to plant trees?

f) What do you think women in each of the cases could
gain from tree growing? Specify what type of tree
growing activity, and expect ed benefits.

g) What constraints are there for women to participate in
tree growing activities (time, lack of land...)?

h) What is the extension message proposed by the
extension worker interviewed in each case, e g what
kind of activities are suggested for women? How
does the extension worker motivate his/her
suggestion?

i) What extension approach is suggested by the
extension worker, e g how are women proposed to be
reached (through women's groups? through
households...)? How does the extension worker
motivate his/her suggestion?

j) Do you agree with this strategy, or should something
else be done.

2. Are any of the cases applicable to your own areas?
Which case? Why?


Maswali ya kujadili


Maswali yafuatayo yanakusudiwa kuwa kama msaada
kwa wale wote wanaotumia Sinema ya Picha kama ni
kifaa cha mafunzo na kufundishia. Ni maswali yanayo-
faa kwa majadiliano katika vikundi vidogo, wakati wa
kuendesha Semina na Mafunzo kwa wafanyakazi wa
Uenezi.


SEHEMU YA KWANZA: UOTESHAJI MITI

1. Jadili na kuchunguza ile mifano mitatu iliyo-
wakilishwa (Mgeta, Dodoma, na Arusha), na taja
kwa kila sehemu:

a) Ni aina gani ya mazao ya miti na misitu haipatikani,
na yaonekana kuhitajika?

b) Ni mila gani zinazohusu uoteshaji na upandaji miti 1)
kwa wanaume 2) kwa wanawake?

c) Ni aina gani ya miti inayopendelewa na wote
(wanawake kwa wanaume)?

d) Je, wanawake wanao uwezo wakutumiamazao yoyote
ya miti wanayohitaji, na wanayotakiwa kuipatia
familiar?

e) Je, kuna haja ya wanawake kupanda miti?

f) Unafikiri ni nini wanawake wanaweza kufaidika
kutokana na uoteshaji miti? Onyesha, ni aina gani ya
uoteshaji au upandaji, na manufaa yanayotegemewa.

g) Ni vikwazo gani vinawazuia wanawake kushiriki
shughuli za uoteshaji miti (muda, kukosa ardhi...)?

h) Ni shughuli gani zinapendekezwa kwa wanawake na
mfanyakazi wa uenezi? Kwa nini anapendekeza
shughuli hizo, na sio shughuli nyingine?

i) Ni mbinu gani za uenezi zinapendekezwa na
mfanyakazi wa uenezi, kwa mfano ni njia gani
inatazamiwa ya kuwafikia wanawake (kutumia
vikundi vya wanawake? kutumia familia...)? Anatoa
sabubu gani kwa kutumia mbinu hizi?

j) Je, unakubaliana na mikakati hii, au kitu kingine
kifanyike?

2. Katikamifano iliyowakilishwakuna wowote unaofaa
kwa sehemu yako? Ni mfano upi? Kwa nini?3. Discuss and analyze your own areas: Answerquestions
1 (a-g) for your area.

h) What extension message (e g what kind of tree
growing activities and what species) would you
suggest for women in your area?

i) What extension approach would you use (e g how
would you reach women)?PART II: SUSTAINABLE USE OF THE
NATURAL FORESTS

Case I Morogoro

1. What is the extension message in this case, e g what
does the extension worker propose should be done
concerning women and forest resources in her area?

2. How does she motivate her suggestion?

3. What is the extension approach chosen, e g how does
the extension worker get her message through, and
which is her most important target group in this case?

4. Discuss and analyze your own areas:

a) Do you have natural forests and woodlands in your
area?

b) How are these presently used by the farmers (men and
women respectively)?

c) Which (if any) of these utilizations contribute to
deforestation?

d) Are there other causes of deforestation in your area?

e) Which utilizations of the forests and woodlands in
your area do not destroy the forests, and could be
allowed to continue?

f) Which utilizations should be forbidden or restricted?

g) Is the strategy suggested in the Morogoro case
applicable in your area? Motivate your answer.


3. Jadilina chunguza sehemu yako yakazi: Jibu maswali
yaliyo katika namba 1 (a-g) kulingana na sehemu
yako.

h) Ni shughuli gani (kwa mfano ukuzaji miche au
upandaji miti, na aina gani ya miti) ungependekeza
kwa wanawake wa sehemu yako?

i) Ungetumia mbinu gani (kwa mfano, ni vipi
ungewafikia wanawake)?


SEHEMUYAPILI: MATUMIZIBORAYAMISITU
YA ASILI

Mfano I Morogoro

1. Shughuli gani za misitu kwa jamii zimependekezwa
katika mfano huu, kwa mfano ni nini mfanyakazi
anapendekeza kifanyike kuhusiana na wanawake na
misitu ya asili katika sehemu yake?

2. Anatoa sabubu gani kwa kupendekeza shughuli hizi?

3. Ni mbinu gani za uenezi zilizopendekezwa, kwa
mfano, ni vipi mfanyakazi wa uenezi anawakilisha
maoni yake, na ni nani hasa anawakusudia?

4. Jadili na kuchunguza sehemu yako:

a) Je, kuna msitu wa asili na nyika kwenye sehemu
yako?

b) Kwa sasa, ni vipi misitu hii inatumiwa na wakulima
(wanawake kwa wanaume)?

c) Ni matumizi gani uliyoyatajahapojuu yanasababisha
kutoweka kwa msitu?

d) Je, kuna sababu nyingine za kutoweka kwa msitu?

e) Ni matumizi gani ya msitu na nyika katika sehemu
yako hayaharibu msitu, na yanaweza kuruhusiwa
kuendelea?

f) Ni matumizi gani lazima yakatazwe au kuzuiliwa?

g) Je, mikakati iliyopendekezwakwaMorogoro yaweza
kutumika katika sehemu yako? Eleza sababu kwa
majibu yako.Case II Improved stoves

1. What kind of improved stoves (charcoal or firewood
stoves) seems to be most popular in Morogoro? Why
are they popular?

2. Discuss and analyze your own areas:

a) Are women asking for firewood saving stoves? If
yes, what reasons do they give? If no, why not?

b) Are women asking for charcoal saving stoves in your
area?

c) If yes: Are they town-living or village women? What
reasons do they give for wanting a charcoal saving
stove?

d) What would be an effective argument (if there is one)
for motivating women to use: 1) firewood saving
stoves 2) charcoal saving stoves?

Case III Traditional Forest Reserves (TFR)

1. What are the laws of the women's TFR in Babati?

2. Why do you think the laws are followed?

3. How does the local forester incorporate the TFR:s in
his own extension work?

4. Discuss and analyze your own areas:

a) Are there any such TFR:s in your area, and are there
different ones for men and for women?

b) If yes, what are the laws of these TFR:s?

c) Could they be a help in your extension work? If yes,
in what ways?


GENERAL QUESTIONS

1. Discuss advantages and disadvantages of working
only with women's groups in your own areas?

2. Discuss advantages and disadvantages of assigning
specific female extension workers the task of working
with women?

3. What does "women participation" mean to you?


Mfano II Majiko sanifu

1. Ni aina gani ya majiko sanifu (jiko la mkaa aujiko la
kuni) ambalo linapendwa sana Morogoro? Kwa nini
yanapendwa?

2. Jadili na chunguza sehemu yako:

a) Je, wanawake wanaulizia kuhusu majiko yanayo-
tumia kuni kidogo? Kama ndio, wanatoa sababu
gani? Na kama sio, kwa nini?

b) Je, wanawake wanauliziakuhusumajiko yanayotumia
mkaa kidogo?

c) Kama ndio, je, wao ni wanawake wanaoishi mjini au
wanaishi kijijini? Ni sababu gani wanatoa kuhusu
kwa nini wanataka jiko linalotumia mkaa kidogo?

d) Ni hoja gani ingefaa kivitendo (kama zipo) ya kuwa-
hamasisha wanawake ili kutumia: 1) jiko linalobana
matumizi ya kuni? au 2) jiko linalobana matumizi ya
mkaa?

Mfano III Misitu ya kimila

1. Ni sheria gani zinahusu misitu ya kimila ya wanawake
Babati?

2. Unafikiri kwa nini sheria zinafuatwa?

3. Ni kwa namna gani Bwana miti analiingiza suala la
misitu ya kimila katika kazi zake za uenezi?

4. Jadili na chunguza sehemu yako:

a) Je, misitu ya kimila ipo, naje, misitu hiyo ipo tofauti
kwa wanawake na kwa wanaume?

b) Kama ndio, misitu hiyo ya kimila sheria zake ni gani?

c) Je, sheria hizo zinawezakusaidiakazi yako yauenezi?
Kama ndio, ni kwa vipi?


MASWALI YA JUMLA

1. Jadili faida na hasara za kufanya kazi na vikundi vya
wanawake tu katika sehemu yako.

2. Jadilifaidanahasarazakuwapangiakazi wafanyakazi
wa kike tu kushughulika na wanawake.

3. "Wanawake kushiriki" ina maana gani kwako?
90. Shukrani kubwa kwa wote wataalam na wakulima,
wanawake na wanaume waliotusaidia kukamilisha
sinema hii.
University of Florida Home Page
© 2004 - 2010 University of Florida George A. Smathers Libraries.
All rights reserved.

Acceptable Use, Copyright, and Disclaimer Statement
Last updated October 10, 2010 - - mvs